Duration 12:54

Hebu Msikie Waziri wa Ulinzi na JKT Dkt. Stergomena Tax Akiongea na Maafisa na Askari Base ya Mwanza

19 709 watched
0
101
Published 21 Dec 2021

Waziri Dkt Stergomena Apongeza Kazi Nzuri inayofanywa na Jeshi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb) amepongeza kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Pongezi hizo amezitoa alipotembelea vikosi na viteule mbalimbali vya Kanda ya Mwanza wakati wa ziara yake aliyoifanya mkoani humo. Mheshimiwa Waziri katika ziara zake vikosini aliweza kupatiwa taarifa mbalimbali kuhusu utendaji kivita, ikama, majengo na miundombinu, miradi mafanikio, mafanikio na mipango ya baadaye. Mbali na taarifa hizo aliweza pia, kutembelea baadhi ya maeneo yakiwemo Hospitali ya Kanda ya Mwanza, ujenzi wa miundombinu, silaha, miradi mbalimbali inayotekelezwa na vikosi hivyo. Akiongea na Maafisa na Askari wa Kanda Mheshimiwa Dkt. Tax amesema kuwa licha ya vikosi kukabiliwa na changamoto katika vikosi hivyo vinapotekeleza majukumu yao, lakini wameendelea kutekeleza kwa bidii jukumu la msingi la kulinda mipaka ya nchi na mafanikio yake yanaanza kuonekana. Aidha, amewasihi kuendelea kuchapa kazi huku wakijua kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu analipenda na kulithamini Jeshi, kwa maana hiyo yupo nao bega kwa bega kuhakikisha changamoto zote zinatatuliwa. Baadhi ya changamoto zimeanza kufanyiwa kazi kwa wakati na kwa uharaka unaotakiwa. Kuhusu kuchukua tahadhali dhidi ya UVIKO -19, Mheshimiwa Dkt. Stergomena amewataka Maafisa na Askari kuendelea kuzingatia maelekezo ya wataalam wa afya kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka, kukaa umbali wa mita moja ikiwa ni pamoja na kuchanja. Pia amewataka kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa UKIMWI maana umeonekana kurudi kwa kasi. Tunapoelekea kusherehekea sikukuu za Kristmas na mwaka mpya, Mheshimiwa Waziri amewatakia Maafisa, Askari, Vijana na Watumishi wa Umma wa Wizara ya Ulinzi na JKT Kristmas njema na kheri ya mwaka mpya.

Category

Show more

Comments - 15