Duration 3:1:8

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA IBADA YA EVENING GLORY - FRIDAY PRAYERS

16 779 watched
0
238
Published 12 Mar 2021

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA IBADA YA EVENING GLORY - FRIDAY PRAYERS 12/3/2021 UJUMBE WA LEO: "NJIA YAKO DUNIANI" "YOUR WAY UPON THE EARTH" NAMNA NGUVU YA KUINUKA TENA INAVYOWEZA KUSHINDA NGUVU YA MATAZAMIO YA WATESI WAKO Matendo 12 : 6 - 19 Ayubu 22 : 29 - 30 Ayubu 14 : 7 - 9 Matendo 12 : 6 - 19 6 Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza. 7 Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi. 8 Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate. 9 Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono. 10 Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha. 11 Hata Petro alipopata fahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi. 12 Na alipokuwa akifikiri haya akafika nyumbani kwa Mariamu, mamaye Yohana, ambaye jina lake la pili ni Marko; na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba. 13 Naye alipobisha kilango cha lango, kijakazi, jina lake Roda, akaja kusikiliza. 14 Alipoitambua sauti ya Petro, hakukifungua lango, kwa ajili ya furaha, bali alipiga mbio, akaingia ndani akawaambia kwamba Petro anasimama mbele ya lango. 15 Wakamwambia, Una wazimu. Lakini yeye akakaza sana, akasema ya kwamba ndivyo hivyo. Wakanena, Ni malaika wake. 16 Petro akafuliza kugonga, hata walipokwisha kumfungulia wakamwona, wakastaajabu. 17 Naye akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Kampasheni Yakobo na wale ndugu habari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine. 18 Hata kulipopambauka askari wakaingiwa na fadhaa nyingi, amekuwaje Petro. 19 Na Herode alipomtafuta, asimwone, aliwauliza-uliza wale walinzi, akaamuru wauawe. Kisha akatelemkia kutoka Uyahudi kwenda Kaisaria, akakaa huko. Ayubu 22 : 29 - 30 29 Hapo watakapokuangusha, utasema, Kuna kuinuka tena; Naye mnyenyekevu Mungu atamwokoa. 30 Atamwokoa na huyo asiye na hatia; Naam, utaokolewa kwa sababu ya usafi wa mikono yako. Ayubu 14 : 7 - 9 7 Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena, Wala machipukizi yake hayatakoma. 8 Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani, Na shina lake kufa katika udongo; 9 Lakini kwa harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi kama mche. Mhubiri : Mwl. Emilian Katubayemo Kwa maombi na ushauri: Mch. Dkt. Eliona Kimaro. Simu :+255655516053, +255754516053 YouTube : Rev. Dr. Eliona Kimaro TV Barua Pepe: elionakimaro555@gmail.com

Category

Show more

Comments - 45