Duration 4:50

CYPRIAN MUSIBA AINGIA MITINI/WAFANYAKAZI WAKE KUMBURUZA KORTINI ANATUFANYIA UHUNI

21 662 watched
0
96
Published 10 Jul 2021

Wafanyakazi wa Kampuni ya CZ Information and Media, wanatarajia kumpeleka mahakamani mmiliki wa kampuni hiyo , Cyprian Musiba, kwa madai ya kutowalipa mishahara miezi mitatu mfululizo. Kampuni hiyo inayomiliki magazeti matatu, Tanzanite, Fahari Yetu na Tanzania Perspective, inadaiwa kutolipa mishahara wafanyakazi wake 68, kuanzia Aprili hadi Juni 2021. Taarifa hiyo imetolewa leo Jumamosi, tarehe 10 Julai 2021 na Mhariri wa magazeti hayo, Mussa Mkama, akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam. Mkama amesema watafungua kesi katika Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi (CMA), Jumatatu ya tarehe 12 Julai 2021, ili kudai haki yao. Mkama amedai kuwa, wamefikia uamuzi huo baada ya Musiba kuingia mitini, tangu Alhamisi ya wiki hii. “Tuna mdai mishahara ya miezi mitatu, Aprili, Mei na Juni na sasa Julai hiyo inaelekea kwenda kukatika. Juzi Jumatano tumezungumza naye vizuri kwamba, Alhamisi tutakaa kufanya kikao na wafanyakazi tujue mustakabali wetu lakini ametufanyia uhuni,” amedai Mkama. 🔘JE, NA WEWE UNA HABARI? 🔘WASILIANA NA MwanaHALISI TV ( +255 767 400402), 🔘WhatsApp ( +255 692 318213) 🔘Email: mwanahalisitvnews@gmail.com 🔘KWA HABARI ZA KILA SIKU: http://mwanahalisionline.com

Category

Show more

Comments - 150