Duration 11:18

NAIBU WAZIRI UCHUKUZI AITAKA MAMLAKA YA BANDARI MTWARA KUSIMAMIA UBORA WA KOROSHO ZINAZOKWENDA NJE

678 watched
0
2
Published 4 Oct 2023

Serikali imeanza rasmi kutekeleza mkakati wa kuhakikisha bandari ya Mtwara inatumika katika kusafirisha zao la korosho na bidhaa nyingine za mazao kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi jambo litakaloinua uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla. Hayo yameelezwa leo (Oktoba 4,2023) na Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile katika Mkutano wa wadau wa zao la korosho kilichofanyika mkoani Mtwara kwa ajili ya maandalizi ya usafirishaji wa zao la hilo kupitia bandari ya Mtwara. Pia Naibu Waziri wa Uchukuzi ameiagiza TPA kusimamia ubora wa korosho inayosafirishwa ili kulinda uthabiti wa soko kwani vinginevyo itakuwa ni hasara kwa taifa. Mkutano huu wa wadau wa korosho ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa alipofanya ziara mwezi uliopita katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo aliagiza korosho kuanza kusafirishwa kwenda nje kwa ajili ya mauzo kupitia bandari hiyo.

Category

Show more

Comments - 1